Naitwa ABRAHAM ALFRED
ni Mkazi wa mfulu Morogoro nina umri wa miaka 56 na kikabila mimi ni Mnyamwezi,
Matatizo yangu yalianza muda kidogo siku moja
nilivyoamka asubuhi nilihisi ganzi katika miguu yangu baada ya siku
kadhaa ganzi hiyo iliendelea hadi kufika Kiunoni hapo ndipo hali yangu ilikuwa
mbaya sana sikuweza kutembea peke yangu vizuri kama zamani, pia hata nilibidi
nisimame kufanya kazi kutokana na matatizo yaliyo nitokea hali ilizidi kuwa
mbaya ndipo nilipo amua kwenda Hospitali ya mkoa Morogoro ili kuchukua vipimo ,
Nilipofika nilipima vipimo vya PRESHA,
HIV na XRAY na baada ya vipimo
niligundulika na magonjwa ya SUKARI ,
PRESHA, FIGO YA KULIA ILIKUWA IMEKUFA, INI HALIFANYI KAZI, Na madaktari waliniambia hata ganzi niliyokuwa nayo
ilisababishwa na hayo magonjwa kwahiyo nilipewa dawa za kutumia lakini
hazikufanya kazi na hali ilizidi kuwa mbaya zaidi , Ndugu zangu wa kristo hapo
ndipo niliamua kwenda kwa waganga wa kienyeji. Nilipita kwa waganga takribani
18 wa hapa Morogoro kujaribu kutafuta msaada wa hali ya afya yangu lakini
nilipoteza Pesa nyingi na sikuona unafuu wowote bali nilizidi kupata shida.
Ndipo siku moja Kuna jirani yangu mmoja alikuja kunihubiria
habari za yesu na kunishauri niende naye katika ibada siku ya ijumaa tarehe
19/02/2016 Nilikubaliana naye na siku hiyo nilikwenda kanisani(EFATHA MINISTRY MOROGORO) Wakati wa
maombezi ulipofika nivyoombewa nilianguka baada ya hapo nilianza kuhisi ile
ganzi miguuni ikianza kuondoka katika miguu yangu. Na ndipo mchungaji (GLADNESS TUPA) Akaniamuru “NITEMBEE”
Niliamka kwa Imani na kuanza kutembea na kukimbia na kucheza nyimbo za dini
zilizokuwa zikipigwa wakati ule, Nilifurahi sana na kumshukuru MUNGU kwa
aliyonitendea “KWAKWELI SITA MUACHA HUYU
YESU.”
NAITWA UPENDO MWAKYUSA: