MCH RICKY MONGI

 

MCH RICK  MONGI

 

SOMO :NGUVU YA UPENDO INAVYOWEZA KUFANIKISHA MAISHA YAKO YA KIMWILI NA KIROHO

Nguvu hii ni mojawapo ya nguvu ambayo huleta matokeo mazuri na hutenda kazi katika ulimwengu wa Roho ,nguvu hii inasababisha huruma ambayo humsukuma mtu kushikamana na  kuambatana na wenye  uhitaji  na ina mfanya mtu kumpenda mtu hatakama amekufanyia mabaya haijalishi amekufanyia nini
nguvu hii ikitenda kazi na hao inasababisha msamahaa kutokea na inazuia nguvu ya dhambi
 mwenye hiyo nguvu ya upendo akiwepo mahali anasababisha watu kupokea msamaha na huruma ya Mungu, mtu mwenye hii nguvu ya pendo akiingia kwenye nyumba ya mtu inafanya hatakama watu hao walikuwa haawaelewani wana patana
upendo ndio unaaongeza kiwango cha upako kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ,yesu alikuwa na upako usio na kikomo kwasababu alimpenda mungu kuliko upeo
mungu anapotaka kumpa mtu cheo au upako , maono , ufunuo wa kutenda miujiza na ishara anmtafuta mwenye upendo ,ukiona umepandishwa cheo basi ndani yako kuna upendo (yohana 3:16)
kukosa nguvu hii ni dalili kwamba haupo karibu na mungu kwa sababu yeye ni asili ya huo upendo , kama hauna huo upendo ni dalili kwamba haupo na Mungu ,nguvu ya upendo huondoa hofu ndani ya mtu , mtu mwenye  hofu hajakamilika katika huo upendo
1 yohana 4:18 – katika pendo hamna  hofu lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu kwamaana hofu ina adhabu na mwenye hofu  hakukamilishwa katika pendo
1 yohana 4:16-17
Kanisa ni mwili wa kristo ,Kanisa likiwa na upendo linakaa ndani ya mungu maana mungu anakaa ndani yake , mwanadamu kwa asili ameumbwa na upendo kwakuwa tumeumbwa kwa sura na mfano wa mungu
1 Korinto 12:26 – na kiungo kimoja kikiumia viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa viungo hufurahi pamoja nacho
Nini kwa kani sa , kanisa ni mwili wa kristo tena huo mwiliuna viungo kila mtu ndani ya kanisa n kiungo kaktika huomwili wa kristo
Rumi 12:4-21
Usishindwe na ubaya bali ushinde ubaya kwa wema  na mpendane ninyi kwa ninyi
v  Huwezi ukampenda MUNGU ikiwa ndugu yako humpendi ambaye nikiungo cha mwili wa kristo
1 Yohana 4:20 -21 ,3:15
Kama unataka kutembea na mungu dumisha upendo, msiwe wanafiki
Nguvu ya upendo ktk kanisa inapelekea bwana kuongeza kanisa na kufanya kanisa kukua
MDO 2:42-47
kama unataka kupona usimshikirie mtu

Share this