ABOUT US

 Huduma ya Efatha mkoa wa Morogoro Ambayo nayo ipo chini ya Mtume na Nabii Josephath Elias Mwingila ambayo inaongozwa na Gladness Tupa ipo maeneo ya Mapumbani barabara mpya iendayo Dar es salaam Jinsi ya kufika hapa ukitoka mjini utapanda Gari za Tubuyu alafu utashuka kituoa cha mapumban hapo ndipo utaona kibao kitakacho kuelekeza mpaka kufika kanisani hapa
KARIBUNI

HISTORIA YA EFATHA
Huduma ya EFATHA yenye msingi wa Kitume na Kinabii, ilianzishwa mwaka 1996 na kuandikishwa kisheria hapa Tanzania mwaka 1997. Huduma hii imeinuliwa kwa majukumu makuu matatu; Moja Kuponya watu kutokana na mateso ya magonjwa na madhaifu mbalimbali. Pili Kuwafungua watu kutoka kwenye vifungo mbalimbali vya mwili, nafsi na roho. Tatu Kuliandaa kanisa la mwisho tayari kwa ajili ya unyakuo. Tumedhamiria kuwafikia wote waliokusudiwa na Mungu kwa njia mbalimbali kama vileTV, Radio, Mitandao ya Kijamii kama Facebook, Twitter, Blog na Youtube. Pia kupitia Ibada, makongamano na warsha mbalimbali. Huduma ya Efatha chini ya mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira, ambaye ndiye Mkurugenzi wa huduma hii, ambayo inaendelea kukua kwa kasi hapa Tanzania na nje ya Tanzania ikiwa na makanisa zaidi ya 200 na makanisa zaidi ya 15 nje ya nchi. Huduma ya Efatha imeanzia Tanzania na kuenea sehemu mbalimbali Afrika na nje ya Afrika. Hadi sasa Efatha ina vituo vya ibada Kenya, Zambia, Malawi, Rwanda, Afrika ya Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Marekani, Ulaya.