PENYE NURU PANA MAJUKUMU


MCH. RICKY MONGI


    Mwaka wa mtembeo wa mng`ao ni mwaka wa kutembea na kuwa na majukumu maana mng`ao ni majukumu hivyo mtu mvivu mzembe asiye  na chakufanya hawezi kung`aa maana penye mng`ao pana majukumu maana kuwa na Mungu nikuwa na majukumu.
Huu sio wakati wa kupoteza muda maana penye nuru pana majukumu , Na kazi ya nuru ni Kuongeza, kustawisha,  kuchanusha.
Mtu wa Mungu ni mtu wa majukumu na nuru ni majukumu na kukubali kutembea na mng`ao ni majukumu
Luka 8:16
                         
Jukumu la nuru ni kuwaonyesha na kuwaangazia wanaoingia wajue cha kufanya
Jukumu ya nuru ni kuwapa ulinzi waingiao hivyo nuru ina majukumu na wewe pia unapaswa kuwa na majukumu
Taa siku zote inawekwa juu kwa sababu ina jukumu la kuangaza na taa isiyoangaza siku zote  inashushwa  jiulize wewe una jukumu gani litakalokufanya uinuliwe juu usishushwe tena?
Mathayo 5:14-16

Maana Mungu wako atatukuzwa kwa jukumu unalolifanya na siku zote hutahitaji kushuhudia maana jukumu lenyewe linamuuza Yesu
Kwasababu wewe ni nuru tena unaangaza kuna vitu utafanya vitakua sababisha wengine kuiga kutoka kwako maana nuru yako inatakiwa kuangaza mbele za watu
Kazi unayoifanya, biashara unayoifanya shuhuli yoyote unayoifnya unapaswa uwe zaidi ya wengine kwasababu wewe ni nuru
Mtu wa nuru ni kiongozi kwa wengine maana nuru huwa inatuongoza
Mtu wa nuru ni mtu wa kuonyesha njia maana nuru inatuangazia
Mtu wa nuru anapaswa kuigwa na wengine
Mtu wa nuru anafanya kitu cha  tofauti na wengine
Mtu wa nuru hapaswi kujidharau, kukiri udhaifu na  kushindwa
Isaya 42:6-7
Kuwafungua macho vipofu yaani kufanya mambo ambayo wengine walikuwa hawayaoni bali sasa wanaona kupitia wewe
YOHANA 11:9-17
Haiwezekani ukafungua biashara au kufanya kitu chochote katika mwaka huu wa mng`ao halafu kikakwama
Leo jiulize lazaro ni kipi katika maisha yako? kipi kimekufa Katika maisha yako? lakini kwa haijalishi chochote ulichonacho kimekufa siku ngapi kwa mamlaka ya jina la Yesu chochote kilichokufa kama lazaro lazima anaenda kufufuka

Share this