SIKU YA KWANZA
Somo: FAMILIA KAMA LANGO
Maana
ya lango
Yohana
10:9
Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi,
ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. Katika Yohana 10:7 Bibia
inasema;“Basi Yesu aliwaambia
tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.”
Kuna mlango ukiingia sahau wokovu na Kuna mlango ukiingia kuna utele, utele
wa Maisha, Baraka, Amani, uzima n.k. Huu ndiyo mlango wa Yesu Kristo.
Tunaweza kuona katika Yohana 10:10;Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka;
ataingia na kutoka, naye atapata malisho. Mtu alivyo nia sawasawa na mlango
alikotokea.
Tuangalie sasa lango katika kiwango cha familia
Mwanzo 49:1-
1.
Yakobo akawaita wanawe, akasema,
Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.
2.
Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo,
Msikilizeni Israeli, baba yenu.
3.
Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu
zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.
4.
Umeruka mpaka kama
maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.
Kuna mambo hayatafutwi chuoni au kwa kuwa
na elimu, bali mtu huyapata katika familia aliyozaliwa, mfano UKUU na NGUVU.
Mwanzo 47:7
Yusufu akamleta Yakobo babaye ndani
akamweka mbele ya Farao Yakobo akambariki Farao.
(Ndivyo ilivyo katika familia zingine,
watu wakuja hubarikiwa na kuacha wa ndani bila mibaraka).
Mwanzo 29:20-25
20. Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama
siku chache tu kwa vile alivyompenda.
21. Yakobo akamwambia Labani, Nipe mke wangu, maana siku zangu zimetimia;
niingie kwake.
22. Labani akakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu.
23. Ikawa wakati wa jioni akamtwaa Lea, binti yake, akamletea Yakobo, naye
akaingia kwake.
24. Labani akampa Lea mjakazi wake Zilpa, awe mjakazi wake.
25. Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii
uliyonitenda?
Hapa tunaweza kuona kuwa katika familia
nyingi ni wengi wameoa akina lea badala ya Raheli, Kutokana na changamoto za
mazingira, masomo, utajiri n.k. watu wamebadili mitazamo yao na kuoa wanawake
wasio wa kwao!!
Angalia familia ya yakobo ilivyoishi
Mwanzo 30:14-15
14. Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano
akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea,
Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao.
15. Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo
kuninyang'anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli
akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao.
Hapa utaona kuwa
familia haikuwa na Amani kutokana na Yakobo kumwoa Lea kwanza badala mke wa
agano lake Raheli.
Siyo sawa kuwalaumu
wazazi maana hujui yale waliyoyapitia mpaka kufikia hapo walipo, maana mtu
huweza kupitia mambo yakambadilisha na kuyafanya yaliyo kinyume na kusudi la
kuumbwa kwake. Tunaona katika mwanzo 30:1-13, ambapo Yakobo alijikuta anakuwa
na wanawake wane badala ya mmoja Raheli aliyekuwa wa agano naye. Maamuzi haya
yalitokana na Yakobo kukosa UTHABITI katika MAISHA baada ya kutendwa. Ndipo
utendaji wake, mawazo yake, maamuzi yake na mfumo wake mzima wa maisha
ulipobadilika hata kufikia kutoa laana kwa mwanae Reubeni.