WAZO LA MUNGU

Bwana asema hivi "Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumbnamna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Yeye achinjaye ng'ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao."
                                                                                                                                         Isaya 66-1- 3
 NB;
katika wazo la Mungu kuna ujasiri ,Katika wazo la Mungu kuna uwezesho
ili uweze kutembea katika wazo la Mungu lazima ukubali  kutembea katika utakatifu
Lazima uonyeshe wazo la Mungu katika maisha yako tena kwa matendo ndipo utakapo weza kuonyesha umuhimu katika wokovu wako.
Utakatifu niwazo Mungu aliwaza
Ukitembea na mng’ao dhambi haita kuweza 
Huu nimwaka wa kung’aa onyesha kuwa umekubali kutembea katika  utakatifu wa Mungu..
Mungu kila siku ana tuwazia mawazo mema
Kama wazo lakimungu limepitishwa kwa mazabau ya Efatha ni  mwaka wakung’aa
Akunachochote kitakachoweza kukuzuia wewe using’ae ila niwewe mwenyewe
Mtu yoyote ambae sio muombaji wazo lamungu halipo ndani yake 
 

SEMINA YA KIROHO

MCH;GLADYNESS TUP
SOMO: KUMILIKIWA NA KUKANDAMIZWA UFAHAMU 
      Kumilikiwa na kukandamizwa kupo kwenye mawazo ya umaskini, kuna wengine sio ni pesa inawafanya washindwe kufanya kazi bali ni umasikini.tamani kujifunza na kuwaza mawazo mazuri
Shida ya watu wengi hawataki kujifunza na kutaka kujua mwenzako anafanyaje ili ufanikiwe. Na pia ujue kwanini ndugu yako anafanikiwa, kama watu tuliookoka tunatakiwa kujifunza
Zaburi 106 33-35.
Unatakiwa uwe tayari kujifunza ubaadae wako na Mungu, shetani anakukamata katika vitu uvipendavyo kama simu ili vikufanye  ushindwa kujifunza elimu ya Mungu. kupo
Haiwezekani ujifunze mambo ya Mungu  na ibu ikakujilia bali siku kwa siku unabadilika kimaneno na kimatendo KWA KUJIFUNZA MAMBO YA MUNGU unakuwa wa tofauti . MTU anayetaka kujifunza mambo ya mungu unakwa watofauti

PENYE NURU PANA MAJUKUMU


MCH. RICKY MONGI


    Mwaka wa mtembeo wa mng`ao ni mwaka wa kutembea na kuwa na majukumu maana mng`ao ni majukumu hivyo mtu mvivu mzembe asiye  na chakufanya hawezi kung`aa maana penye mng`ao pana majukumu maana kuwa na Mungu nikuwa na majukumu.
Huu sio wakati wa kupoteza muda maana penye nuru pana majukumu , Na kazi ya nuru ni Kuongeza, kustawisha,  kuchanusha.
Mtu wa Mungu ni mtu wa majukumu na nuru ni majukumu na kukubali kutembea na mng`ao ni majukumu
Luka 8:16
                         
Jukumu la nuru ni kuwaonyesha na kuwaangazia wanaoingia wajue cha kufanya
Jukumu ya nuru ni kuwapa ulinzi waingiao hivyo nuru ina majukumu na wewe pia unapaswa kuwa na majukumu
Taa siku zote inawekwa juu kwa sababu ina jukumu la kuangaza na taa isiyoangaza siku zote  inashushwa  jiulize wewe una jukumu gani litakalokufanya uinuliwe juu usishushwe tena?
Mathayo 5:14-16