MCH RICKY MONGI

 

MCH RICK  MONGI

 

SOMO :NGUVU YA UPENDO INAVYOWEZA KUFANIKISHA MAISHA YAKO YA KIMWILI NA KIROHO

Nguvu hii ni mojawapo ya nguvu ambayo huleta matokeo mazuri na hutenda kazi katika ulimwengu wa Roho ,nguvu hii inasababisha huruma ambayo humsukuma mtu kushikamana na  kuambatana na wenye  uhitaji  na ina mfanya mtu kumpenda mtu hatakama amekufanyia mabaya haijalishi amekufanyia nini
nguvu hii ikitenda kazi na hao inasababisha msamahaa kutokea na inazuia nguvu ya dhambi
 mwenye hiyo nguvu ya upendo akiwepo mahali anasababisha watu kupokea msamaha na huruma ya Mungu, mtu mwenye hii nguvu ya pendo akiingia kwenye nyumba ya mtu inafanya hatakama watu hao walikuwa haawaelewani wana patana


Wana wa mungu wa EFATHA MOROGORO wakiwa ibadani kumwabudu, kumsifu na kusikiliza neno la mungu ili liweze kuwatoa mahali
Mchungaji kiongozi Gladyness Tupa wa Efatha Morogoro

MAHUBIRI


MCH GLADYNESS TUPA


Kutoka 15:26-akawaambia kwamba utaisikiza sauti ya bwana Mungu wako na kuyafanya yaliyo elekea mbele zake ,na kutega masikio usikize maagizo yake, na kuzishika amri zake mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia wamisri; kwa kuwa mimi ndiye BWANA nikuponyaye.
Mungu anawaambia wengi Lakini mmoja tu ndiye anayepaswa kusikia,Jifunze kusikia mara moja na lazima umkumbuke Mungu anaye kupa nguvu usipo mkumbuka sahau utajiri wako (kumb 8: 18), ukiona upo kanisani unasinzia au unaongea yasiyofaa ibadani jua hofu ya Mungu imeondoka ndani yako ,na Yule mtu ambaye ni mvivu kusoma neno mara zote anasinzia ibadani
(tiisha kila kiungo cha mwili wako kabla ya kuingina ibadani ili visikucheleweshe maana huu ni mwaka wa kukaa barazani pa Mungu na sio pa wenye mizaa na kunena yasiyofaa kwenye ulimi wako zaburi 1:1)
Wewe umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na mawazo akuwaziayo ni mema na ukishika sheria ya bwana amani ya mungu ipo pamoja na wewe maana Mungu anataka kutembea na wewe katika mwaka huu 2015 , usipo weza kutembea na Mungu na kama hutaweza kutembea na roho mtakatifu mwaka huu huwezi kumshinda shetani , kuishinda dhambi , umasikini na magonjwa, wewe uliyefanya dhambi alafu unakaa pamoja na wana wa mungu wewe ni mmoja wa kuzuia nguvu ya mungu mahali hapo na mungu anakuona Mungu hadhiakiwi

* Siku yoyote unapoamua kufanya Maombi (unafanya maombi ili nini?) , unapofanya maombi yaaina yoyote dhamiria kumshinda shetani katika hayo maombi. kama huja mshinda shetani huwezi kupata majibu ya maombi uliyo ya omba. natakiwa nifanye maombi kwa kudhamiria ili nimshinde shetani na unapofanya maombi ni lazima umalize kazi zote za adui ndani yako mwenyewe iwe ni dhambi , udhaifu au chochote kinacho pingana na utaratibu wa MUNGU. maana adui wa kwanza ni wewe mwenyewe na adui mkubwa kwa mtu ni tabia yake mwenyewe iwe kwa mawazo,maneno au matendo yoyote yaliyo ndani yake mwenyewe maana yeye anajua.
  • Ukifanikiwa kumaliza kazi za adui katika ulimwengu wa roho basi umeshinda na ili umalize ni lazima uwe mtu wa kusamehe yaliyopita na aliye kukosea wakati mwingine unakuwa na tatizo ni kwa sababu hujasamehe, jifunze kusamehe ili nguvu ya mungu ikae na wewe ili iweze kuishinda nguvu iliyo katika ulimwengu wa roho na kazi za ibilisi ndani yako
  •   Natakiwa kuwa na neno la mamlaka la kuishinda hiyo nguvu ili mamlaka ya mungu kila wakati ifanye kazi ndani yako. uwe na tabia ya kujikagua njia zako au kila siku je unachofanya kipo sawa au kina mfurahisha mungu? Neno lolote unalo tamka linamfanya shetani ajue wewe si mali yake na kwakujikagua tu unaweza ukafukuza magonjwa katika mwili wako

Kutoka 23:25-
Mkabidhi bwana njia zako na mawazo yako yaka thibitike kwako , sababu biblia inasema walipokataa kufuata mawazo ya mungu, mungu aliwaacha wafate akili zao zisizofaa , tabia ulizonazo usiendelee nazo mwaka huu 2015 maana mwaka huu ni mwaka wa kutembea na mungu nilazima ukubali kubadilika.

Isaya 33:24 wala hapana mwenyeji atakayesema, mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.
Mawazona matendo yako jitahidi kujionyesha kwamba umekubaliwa na Mungu

Kwanini ahadi alizo kuahidia mungu nyingi hazija timia mpaka leo?
  • Ni kwasababu hujakubali kutii na pia kubali kuongozwa na Roho mtakatifu (ISAYA 1:19 kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi )
mimi ninatakiwa nisizitegemee akili zangu mwenyewe